Halmashauri ya Wilaya ya
Muleba imefanikiwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu
wa zaidi ya kilomita 0.56 katika Kijiji cha Katembe, Kata ya Nyakabango, kwa
kutumia fedha za mapato ya ndani kiasi cha Shilingi Milioni 299,608,500.
Mradi huu unasimamiwa na
Wakala wa barabara za vijijini na mijini Tanzania (TARURA) huku lengo la mradi
huu likiwa ni kuboresha miundombinu ya
barabara kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa samaki na dagaa ili kuongeza
pato la Wilaya na Taifa kwa jumla.
Hadi sasa Mradi huu
umefikia 99% za utekelezaji wake na umegharimu kiasi cha Shilingi milioni
299,608,500 huku kazi zilizobakia zikiwa ni
ufungaji wa taa za barabarani na uwekaji wa alama za vivuko vya watembea
kwa miguu, ili kuhakikisha usalama na matumizi bora ya barabara hiyo.
Hata hivyo Mradi huu
unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wakazi 50,000 kutoka katika kata za Mazinga,
Ikuza na Nyakabango, pamoja nakunufaisha
wafanyabiashara wa dagaa na samaki kutoka mataifa jirani ya Uganda,
Rwanda na Burundi.
Uboreshaji huu wa
barabara unatarajiwa kuchangia kwa kiasi
kikubwa pato la Taifa Wilaya na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.
@ortamisemi
@kagerayetuofficial
@kagera_rs
0 Maoni