Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akiongoza kikao cha kawaida
cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, leo Julai 14, 2025 katika
Ofisi za Makao Makuu ya CCM (White House) mkoani Dodoma.
Kikao hicho,
kinachotarajiwa kuendelea hadi Julai 16, kimeitishwa kufuatia kukamilika kwa
zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi wa nafasi za
uwakilishi katika vyombo vya dola. Nafasi hizo zinahusisha ubunge wa majimbo,
ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, viti maalum vya ubunge na Baraza la
Wawakilishi, pamoja na udiwani wa kata na viti maalum.
0 Maoni