Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene Isaka amesema Mfuko
utashirikiana katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote
na vyama mbalimbali vya kitaalam ili kuwezesha utoaji wa huduma ulio bora
zaidi.
Dkt. Isaka ameyasema
hayo jana wakati akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Kisayansi la Chama cha
Madaktari Tanzania lililolenga kuadhimisha miaka 60.
Alisema kuwa kazi
kubwa iliyofanywa na Mfuko katika maandalizi ya utekelezaji wa Bima ya Afya kWa
wote ni ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wakiwemo madaktari kupitia vyama
vyao.
“Tulianza na utoaji
wa elimu kwa wadau muhimu ambayo iliambatana na kupata maoni ya namna gani
huduma zitolewe na huduma zipi kwa wanachama, pamoja na kukamilisha hili lakini
tutaendelea kushirikiana nanyi na wataalam wengine ili utoaji wa huduma kwa
wanachama wetu uwe bora zaidi.”
Katika hatua
nyingine, Dkt. Isaka alitoa wito kwa wadau hao kulinda huduma na kutojihusisha
na vitendo vya udanganyifu wakati wakitoa huduma kwa wanachama wa NHIF.
Kwa sasa Mfuko
unaendelea na usajili wa Wanachama wake kupitia kifurushi cha Tarangire ambacho
kimeboreshwa kwa kuongezwa huduma mbalimbali za msingi na za kitaalam zaidi.
0 Maoni