Mhe. Naibu Waziri wa
Mali Asili na utalii Mhe. Dustan Kitandula (Mb) jana Juni 20, 2025 alitembelea banda
la NCAA lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Mali asili na Utalii kwenye
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma katika
Viwanja vya Chinangali Park.
Akiwa ndani ya Banda
hilo, Mhe. Kitandula ametoa wito kwa NCAA kuendelea kutoa Elimu kwa umma
kuhusiana na jamii inayoishi ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa kulezea
historia na asili halisi ya jamii hiyo.
Aidha, Naibu Waziri
amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea banda hilo la Wizara ya
Maliasili na Utalii ili kupata elimu kuhusu shughuli za uhifadhi pamoja na
fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana katika sekta ya utalii.
Maadhimisho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma kwa mwaka huu yalianza rasmi Juni 16, 2025, na yanatarajiwa
kufikia kilele chake Juni 23, 2025, yakihusisha taasisi mbalimbali za umma
zikiwemo zile zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
0 Maoni