Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), CPA (T) Musa Nassoro Kuji leo Juni 30, 2025 amekagua miradi ya maendeleo iliyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Mikumi akiwa katika mwendelezo wa ziara zake za kikazi katika Hifadhi za Taifa zilizopo Kanda ya Mashariki.
Miradi iliyokaguliwa
ni pamoja na Lango la kuingilia watalii la Doma ambalo lipo mbioni kukamilika,
Kituo cha kutolea taarifa kwa wageni (VIC), Mradi wa eneo la kupumzikia wageni
na kula chakula cha mchana (Picnic Site), Mradi wa uwanja wa ndege ambao
umefikia zaidi ya asilimia 90 ili ukamilike,
Mradi wa kambi ya kulala watalii pamoja na mradi wa nyumba za kulala
wageni (Bandas).
Kamishna Kuji
anatarajiwa kufanya kikao na watumishi ili kupata taarifa ya utendaji kazi,
changamoto na mafanikio. Aidha, pia atatoa muelekeo mpya na mikakati ya namna
bora ya kuimarisha uhifadhi wa maliasili ndani ya hifadhi hiyo.
0 Maoni