Naibu Waziri Mkuu na
Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Bukombe amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea Ubunge katika Jimbo la
Bukombe.
Dkt. Biteko amechukua
fomu hiyo na kuirejesha kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe,
Ndugu. Leonard Yesaya Mwakalukwa mapema leo Juni 29, 2025.
Zoezi la uchukuaji
fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) linaendelea nchi nzima ambapo
watia nia tofauti wameendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchukua fomu za
Ubunge na Udiwani.
0 Maoni