Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameshiriki katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa Taasisi, Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo Serikali ina hisa zake.
Hafla hiyo imefanyika
leo Juni 10, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam na gawio kupokelewa na mgeni rasmi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan.
Akiongea kwa ufupi kabla ya
kumkaribisha Rais kuongea, Dkt. Biteko amemshururu Rais Dkt. Samia kwa maono yake
yaliyofanikisha siku ya leo Taasisi, Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo
Serikali ina hisa zake kutoa gawio.
0 Maoni