Filamu ya The Royal Tour imezidi kuleta matokeo chanya
katika sekta ya Utalii kutokana na mwamko mkubwa kwa wawekezaji hususan wa
Hotel za kitalii kuendelea kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali hasa kwenye
Hifadhi za Taifa ili kwendana na kasi kubwa ya
watalii wanaoingia nchini.
Akizungumza baada ya kutembelea Hoteli ya Serengeti Explore
by Elewana na Hoteli ya Serengeti Lake Magadi, Mkoani Mara, Katibu Mkuu Wizara
ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesema ujenzi wa Hoteli hizo ni
mwitikio wa kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuinua sekta ya Utalii hasa kupitia Filamu ya
“Tanzania-The Royal Tour,” ambayo imechagiza zaidi kuleta wageni wengi na kufungua fursa zaidi kwa wawekezaji kuwekeza
katika malazi.
Aidha Dkt. Abbasi ameendelea kutoa wito kwa wawekezaji
kuchangamkia fursa adhimu kuwekeza kwa
kujenga hoteli katika hifadhi za kusini ikiwa ni mkakati wa Serikali katika
kuifungua zaidi Kusini pamoja na
kutangaza vivutio vipya vya utalii.
Hoteli ya Serengeti Explore ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100 na Lake Magadi ambayo ujenzi wake unaendelea kwa jumla zina vyumba 150, hivyo zinaongeza zaidi wigo wa Hoteli za Kitalii katika kuwahudumia wageni wengi zaidi wanaoingia nchini.
0 Maoni