Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ni
miongoni kwa washiriki wa Maadhimisho ya
Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) Mkoani Arushs inayofanyika Mei 1, 2025,
katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Aidha, watumishi wa
TAWIRI wameonesha umahiri wao kupitia
maandamano ya miguu na pia kupitia gari la maonesho, ambalo lilikuwa moja ya
vivutio vikubwa katika maandamno haya,
ilikuwa ni fursa kubwa kwa
wafanyakazi wa TAWIRI kunadi mchango wa taasisi katika uhifadhi wanyamapori nchini .
Kupitia machapisho, vipeperushi, video na sanamu za
wanyamapori, TAWIRI ilidhhirisha mbele ya mgeni
rasmi na umma wa Arusha namna tafiti zake zinavyosaidia kuelimisha na
kutatua changamoto za uhifadhi ili kuwezesha maendeleo endelevu ya sekta ya
utalii, na maisha bora ya Jamie.
Kitaifa, maadhimisho ya Mei Mosi, 2025 yanafanyika mkoani Singida, ambapo Mgeni Rasmi ni Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Maoni