Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, amewasihi
Watanzania kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuilinda na kuitunza
miundombinu ya treni ya kisasa ya Umeme (SGR).
Prof. Mbarawa, ametoa wito huo katika stesheni ya Magufuli
Dar es Salaaam, muda mchache baada ya kumsindikiza Rais wa Msumbiji Fransisco
Chapo, aliyesafiri kwa SGR kutoka Stesheni ya Magufuli kwenda stesheni ya Pugu
na kisha kurejea stesheni ya Magufuli, kwa lengo kushuhudia mradi huo ambao ni
wa kilelezo barani Afrika.
Waziri wa Uchukuzi amesema Rais Chapo, aliyeko nchini kwa
ziara ya kiserikali ya siku tatu aliyoaianza Mei 07, 2028 ameeleza kufurahishwa
na mradi huo aliosema ni wa kiwango cha dunia na kuwataka Watanzania, kuulinda
kwa wivu.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw. Masanja
Kadogosa, alisema kuwa ujio wa Mhe.
Chapo ni ishara tosha ya kwamba Afrika inajua nini kinachoendelea Tanzania na
pia kuzidi kudumisha mahusiano baina ya nchi za Afrika na kuimarisha katika
ufanyaji biashara kwa ukaribu.
“Kikubwa zaidi katika nchi za Afrika ni kufanya biashara na wenzetu wa nchi nyingine wanatutazama tofauti, na nchi ya Msumbiji tumekua tukishiriana katika Nyanja mbalimbali ikiwemo siasa, ulinzi na vilevile kijamii ukizungumza mmakonde wa Msumbiji na Tanzania hawana tofauti,” alisema Ndugu Kadogosa.
0 Maoni