Katika shamrashamra za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, yaliyofanyika katika Uwanja wa Nguzo Nane wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Comrade Kenani Kihongosi, alikabidhi cheti cha heshima kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bi. Zahara Muhidin Michuzi, kwa kutambua mchango wake mkubwa kama mfanyakazi hodari na mwenye weledi.
Bi. Zahara alihamishiwa wilayani Meatu mwishoni mwa mwezi
Januari mwaka huu, akitokea Wilaya ya Kilombero Halmashauri ya Mji Ifakara
mkoani Morogoro, ambako pia alihudumu
kama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji huo. Kabla ya hapo, alikuwa
Mkurugenzi wa Mji Geita katika Wilaya ya Geita, Mkoa wa Geita akifanya kazi kwa
bidii na uadilifu uliotambuliwa na wengi na kuacha alama zisizosahailika.
Tuzo hiyo imetolewa kama sehemu ya kuthamini juhudi za
viongozi na watendaji wanaoonyesha juhudi, kujituma, uzalendo wa kweli, ufanisi
na uongozi thabiti katika utumishi wa umma, hasa katika, kusimamia miradi
maendeleo, ukusanyaji wa mapato, kutatua kero za watumishi na wananchi kw
ujumla sambamba na kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yao ya kazi.
Katika hotuba yake, Comrade Kihongosi aliwasihi watumishi wa umma kote mkoani Simiyu kuiga mfano wa Bi. Zahara kwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha alama nzuri zisizofutika, uwajibikaji na moyo wa kizalendo.
0 Maoni