Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mhe. Mary Pius Chatanda ameshuhudia utiaji saini wa mikataba mitano ya bilioni 13.3 zilizotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ili kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja wilayani Rufiji, huku Mhe. Mchengerwa akizindua rasmi Ligi ya ”Mchengerwa Mtu Kazi” inayoanza leo Mei 8, 2025 na kutoa vifaa (jezi na mipira) kwa timu zote 169 kutoka kwenye kata 13 zinazoshiriki mashindano hayo vyenye gharama ya milioni 67 pamoja na fedha taslimu milioni 25 ikiwa ni zawadi za washindi.
Tukio hili la utiaji saini limefanyika jana Mei 7, 2025 mara
baada ya kukamilika kwa ziara ya siku mbili ya Mhe. Chatanda kukagua
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo, katika eneo la
uwanja wa stendi wa Ikwiriri na
kushuhudiwa na maelfu ya wananchi wa wilaya hiyo huku wasanii kadhaa wakitumbuiza kwa
burudani za muziki.
Akitoa taarifa ya miradi hiyo, Meneja wa Wakala za Barabara
Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Pwani, Leopold Runji amefafanua kuwa
gharama hizo zinahusisha ukarabati wa barabara ya Nyamwage yenye Kilomita 28,
ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Chumbi- Kiegele yenye kilomita 1.4,
ukarabati wa barabara ya Mohoro- Mtanga kilomita 12.3 na Mohoro Ndundutawa
yenye kilomita 7.5.
Pia ukarabati wa barabara ya Nyamwage - Mpakani- Nambunju na
ujenzi wa barabara za lami katikati ya
mji wa Ikwiriri ambapo amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kuiunganisha
wilaya hiyo na maeneo mbalimbali
ya mikoa ya Tanzania.
Mhe. Chatanda amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za
miradi na kufafanua kwamba kwa kufanya
hivyo siyo tu ametekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa mafanikio makubwa
bali ameleta mapinduzi
katika sekta ya miundombinu kote nchini.
Amempongeza Mhe. Mchengerwa kwa kusimamia utekelezaji wa
miradi yote kwa kiwango cha juu huku akitoa wito kwa maeneo
mengine nchini kuiga utekelezaji huo.
”Ndugu zangu hapa ni vema tuwe wakweli, unaweza
ukaletewa fedha za maendeleo
lakini ukashindwa kutekeleza lakini,hivyo nampongeza mbunge wenu kwa kusimamia utekelezaji wa
miradi hii ambayo inakwenda kuleta tija kubwa kwa wananchi katika Wilaya ya Rufiji,” amefafanua Mhe.
Chatanda.
Mbali na kukagua miradi
ya Serikali pia ameshuhudia ujenzi wa
nyumba ya mtumishi wa chama, pia
ameshuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa wilaya unaogharimu zaidi ya shilingi
bilioni 2.5 unaofadhiliwa na Mbunge wa Rufiji Mhe. Mchengerwa kwa kupitia
marafiki na wadau mbalimbali.
Akizungumzia kuhusu miradi ya elimu katika wilaya hiyo, Mhe.
Chatanda amesema amefurahishwa na kazi nzuri ya ongezeko kubwa la Shule za
Msingi na Sekondari na kutoa wito kwa wananchi kuwapeleka watoto wao katika shule
hizo ili kuunga mkono maono ya
Mhe. Rais ya kuwakomboa wananchi kielimu pia kwa manufaa makubwa ya taifa na
vizazi vyao.
Mbunge wa Rufiji Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa Serikali imefanya kazi kubwa ya ujenzi wa shule ambapo
amesema wakati anaingia kwenye ubunge
kulikuwa na na Shule za Msingi 40 tu
ambapo sasa kuna shule 63 na upande wa Vituo vya Afya, awali kulikuwa na vituo 3 na sasa vimefika 9, huku asimshukuru Mhe. Rais Samia
kwa maono makubwa ya kuwaletea maendeleo
watanzania.
Aidha, Mhe. Chatanda alipotembelea na
kukagua ukarabati wa hospitali ya
Wilaya ya Rufiji na ujenzi wa kichomea
taka katika eneo la Utete uliogharimu
takribani milioni 900 na kuwataka
wananchi kutumia huduma hizo
ikiwa ni pamoja na wanaume kuwa msitari wa mbele kuwapeleka wake zao kwenye
huduma za kliniki ili kujua afya za wenza wao na watoto.
Akizungungumzia kuhusu ukatili wa kijinsia, amewataka
wazazi kuwalea watoto wao katika misingi
maadili ili waweze kuja kuwa wazazi
bora badala ya kuwaacha kujifunza
kwenye mitandao.
Wakati huo huo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura huku akisisitiza kuchagua CCM kwa kuwa ndicho chama kilichowaletea maendeleo.




0 Maoni