Mhe. Chana awasili Kisarawe kuzindua mradi wa kuhifadhi misitu

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amewasili wilayani Kisarawe mkoani Pwani kwa ajili ya kuzindua mradi wa “Kuimarisha Ustahimilivu wa Bioanuai ya Misitu ya Mazingira Asilia Tanzania dhidi ya Athari za Mabadiliko ya Tabianchi,” na “Mkakati wa Kuongoa Ardhi ya Misitu Iliyoharibika.”

Mhe. Chana amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe.Abubakar Kunenge, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Petro Magoti, Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Wilaya ya Kisarawe, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Uzinduzi huo unafanyika leo Mei 5, 2025 katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Pugu/Kazimzumbwi, Kisarawe Mkoani humo.




Chapisha Maoni

0 Maoni