Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaanza kujenga jengo la kisasa la Makao Makuu ya chama hicho jijini Dodoma linalojengwa karibu na Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka Jiwe la Msingi la Jengo la Makao Makuu ya CCM Mei 28 mwaka huu, amesema CPA Makalla.
CPA Makalla, ameyasema hayo alipokuwa akuzungumza na vyombo vya habari jiji Dodoma Mei 24, 2025, kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu maalumu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
CPA Makalla amesema kuwa Jengo hilo litakuwa la kisasa ambalo litakuwa na huduma zote muhimu na litaendana na hadhi ya CCM ambayo kwa sasa inawanachama zaidi ya milioni 11.
“Tunajenga jengo la Makao Makuu karibu na Jengo hili (Jakaya Kikwete) ambalo litakuwa na facilities zote CCM ni chama kikubwa Tanzania pamoja na Afrika, tumeona umefika wakati wa kuwa na jengo lenye huduma zote kumbi za mkutano, parkingi,”amesema Makalla.
Aidha, amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya Mkutano Mkuu maalumu wa CCM yamekamilika na unatarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na utahudhuriwa na wajumbe 2000 wa mkutano Mkuu kutoka mikoa yote nchini.
0 Maoni