Kashmir pachafuka tena, India na Pakistan zatwangana

 

Nchi za India imefanya mashambulizi ya anga nchini Pakistan huku mataifa hayo yakitoa taarifa zinazokinzana kuhusiana na vifo vilivyotokana na mashambulizi hayo.

India imesema raia 10 wamekufa kwenye mashambulizi iliyofanya upande wa Kashmir uliochini ya Pakistan, huku Pakistan yenyewe ikisema watu 26 wamekufa na wengine 46 wamejeruhiwa.

India imesema imerusha makombora katika maeneo tisa ya eneo la Kashmir lililochini ya utawala wa Pakistan, ambalo wakazi wake waliamshwa na milio ya milipuko mikubwa.

Pakistan imesema kwamba maeneo sita yameshambuliwa, na kudai kwamba wamezitungua ndege sita za kivita za India. India bado haijathibitisha hili.

Hali ya uhasama baina ya mataifa hayo yanayomiliki silaha za nyuklia imeongezeka baada ya mwezi uliopita wanamgambo kushambulia watalii India huko Pahalgam.

Upande wa Kashmir uliochini ya utawala wa India, umekuwa ukishuhudia machafuko yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu. India na Pakistan zote zinamiliki Kashmir yote.

Chapisha Maoni

0 Maoni