Wananchi Mkoani Morogoro wamehimizwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa ili kuepuka usugu unaoweza kusababishwa na matumizi holela bila ushauri wa daktari.
Wito huo umetolewa Mkoani Morogoro na Mfamasia kutoka
Manispaa ya Morogoro Adam Said wakati akitoa elimu ya Afya kuhusu matumizi
sahihi ya dawa kwa waendesha bodaboda na bajaji(JUWATA) ,Wafanyabiashara wa
Soko la Mawenzi pamoja na Stendi ya Mkoa wa Morogoro ikiwa ni katika
utekelezaji wa kampeni ya kuelimisha umma iliyoratibiwa na Baraza la Famasi
Tanzania kwa kushirikiana na Elimu ya
Afya kwa Umma katika utoaji wa Elimu ya Afya.
"Tusiende kununua dawa bila kupima na ushauri wa
daktari inaweza kutengeneza usugu wa dawa," amesema.
Kwa upande wake Mfamasia
Mwandamizi kutoka Baraza la Famasi Tanzania Bi.Anna Temu amesema ni muhimu kufanyiwa uchunguzi kwanza
kabla ya kujinunulia dawa huku akisisitizia kwenda kwenye maduka ya dawa
yanayotambulika na Baraza la Famasi Tanzania.
"Unapokwenda kwenye duka la dawa hakikisha umefanyiwa
uchunguzi kwanza kutoka kituo cha huduma za
afya na pia hakikisha duka la dawa unaloenda kupata huduma liwe
limesajiliwa na Baraza la Famasi," amesema.
Nao baadhi ya Wananchi Mkoani Morogoro wamesema elimu ya
afya imewasaidia kwa kiwango kikubwa kuhusu matumizi sahihi ya dawa.
"Nashukuru kwa elimu niyoipata na nimetambua kuwa hatupaswi kujinunulia dawa bila vipimo na tusiende kwenye maduka yasiyotambulika, twende kwenye maduka yaliyosajiliwa na Baraza la Famasi, " amesema Majaliwa John.
0 Maoni