Mtendaji Mkuu
wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) amewataka wafanyakazi wa
Wakala huo kuwekeza nguvu katika kuwahudumia wananchi.
Ameyasema
hayo jana tarehe 4 Aprili , 2025 wakati akifungua mkutano wa Baraza la
Wafanyakazi wa TARURA linalofanyika katika ukumbi wa Masiti mkoani Iringa.
Mhandisi Seff
amesema kwamba kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano italeta ufanisi na
kuendelea kulinda taswira ya Wakala huo.
Hata hivyo
Mtendaji Mkuu huyo ameahidi kusimamia yale yote yatakayoamuliwa katika mkutano
huo na kuyafanyia kazi kwa ufanisi.
Naye,
Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutoka TUGHE Bw. Mudathiri Ismail amewapongeza TARURA
kwa namna walivyojipanga kutoa elimu hususan yauwekezaji kwa wafanyakazi pia
amewataka wajumbe kuishauri vizuri
menejimenti ili TARURA izidi kusonga mbele kwani inawagusa wananchi moja kwa
moja.
Wakati huohuo
Mwakilishi wa Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Bi. Eunice Tesha ameipongeza TARURA kwa kujua dhana ya
ushirikishwaji kwani mkutano huo ni fursa pekee ya kuwasilisha na kutoa maoni
na kujadili kwa ustawi wa Wakala.



0 Maoni