Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus
Balile amesema uzinduzi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ni mwanzo wa
kupatikana kwa Baraza Huru la Habari hapa nchini.
Akitoa salamu za TEF wakati wa uzinduizi wa Bodi ya Ithibati
ya Waandishi wa Habari, Balile amesema kukiwa na Baraza Huru la Habari
usimamizi wa kazi za wanahabari utakuwa rahisi, na hata kesi zinazohusu taaluma
hiyo zitaamuliwa na Baraza na sio mahakamani tena.
Amesema Baraza Huru la Habari litarahisisha usimamizi wa sekta ya habari na litalinda maslahi ya waandishi wa habari dhidi ya watu wenye nia ovu na sekta hiyo.

0 Maoni