Tanzania yang'aa ITB Berlin 2025

 

Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa  na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb), wameungana na taasisi za sekta ya utalii na zaidi ya wakala 46 kutangaza vivutio vya Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya ITB Berlin 2025.

Maonesho haya, yanayovutia zaidi ya wageni 100,000 na waoneshaji zaidi ya 5,800 na mataifa zaidi ya 170. Hii imekuwa fursa kubwa kwa shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kunadi vivutio na shughuli za utalii zinazofanyika  katika hifadhi  za Taifa pamoja na fursa za uwekezaji. 


         Karibu Tanzania, Karibu Hifadhi za Taifa Tanzania.


Chapisha Maoni

0 Maoni