Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe.
Ridhiwani Kikwete amelieleza bunge Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mikakati
mitano inayofanywa na Serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana
nchini na namna kumudu ushindani kwenye soko la ajira.
Mhe. Kikwete amesema
hayo leo Februari 10, 2025 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpendae
(CCM), Mhe. Toufiq Turky aliyehoji kuna mpango gani wa kuwandaa vyema vijana
waweze kushindana katika soko la ajira ndani na nje ya Tanzania ili kukabiliana
na upungufu wa ajira nchini.
Akijibu swali
hilo, Waziri Kikwete ametaja mipango ya serikali katika kuwaandaa vijana ili
kumudu ushindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Mhe.
Ridhiwani amesema, mipango hiyo ni pamoja na kubuni na kutekeleza programu
maalum zinazowawezesha vijana kujifunza kwa vitendo kupitia sekta zinazozalisha
ajira kwa wingi kama vile sekta ya kilimo kupitia programu ya Jenga Kesho
iliyobora (BBT), ujasiriamali, na madini kupitia Programu ya Mining for a
better Tommorrow (MBT).
Aidha, amesema
kufanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Tolea la Mwaka 2023
ambayo yanasisitiza mafunzo kwa kuandaa wataalamu.
“Kupitia
ujenzi wa miundombinu ya Kimkakati muhimu inayochochea uchumi, vijana
wameajiriwa na kunufaika na urithishwaji ujuzi kutoka kwa wataalamu wa nje
mfano ujenzi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere na barabara za mwendokasi
(BRT),” amesema Mhe. Kikwete.
Pamoja na
mambo mengine, amesema Serikali itaendelea kubuni na kutekeleza programu ya
kukuza ujuzi ambayo inalenga kukuza ujuzi kwa nguvu kazi ili kuwezesha vijana
kushindana katika soko la ajira mfano mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi
waliopo kazini na kwa wajasiriamali.
Mikakati
mwingine ni kuweka msisitizo kwenye matumizi ya TEHAMA katika kuzalisha fursa
nyingi za ajira kwa vijana, amesema Mhe. Kikwete.
0 Maoni