Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA)
limeichagua Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kuhudumia watumishi wake waliopo
Kanda ya Kati na mikoa ya jirani.
BMH inahudumia wananchi takribani 248,260 kwa mwaka kwa
wagonjwa ambao ni wagonjwa wa nje na wa ndani kutoka Kanda ya Kati na mikoa ya
jirani ambayo ni Iringa, Mbeya, Manyara, Tabora, Kigoma na Morogoro.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dkt Kessy
Shija, haya yanafuatia ziara ya ujumbe wa JICA Hospitalini hapa siku ya
Jumatano hii.
"Ujumbe wa JICA umekuja BMH kuangalia huduma baada ya kuichagua BMH kuwa Hospitali ya kuhudumia raia wao waliko Kanda ya Kati," amesema Dkt Shija baada ya kukutana na ujumbe wa JICA ukiongizwa Mshauri wa Masuala ya Afya wa JICA, Bi Pascalina Kiria.
Na. Jeremiah Mbwambo- Dodoma
0 Maoni