Mamba anayesadikiwa kuua watu wakati wa
shughuli za kibinadamu ndani ya Ziwa Victoria, Kijiji cha Kasenyi, Kata ya
Kasenyi, Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, ameuwawa na wananchi kwa kumtenga
kwa kutumia ndoano.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kasenyi, Juma
Bupamba, amethibitisha kuuawa kwa mamba huyo ambaye alikuwa tishio kwa wananchi
wa Kata hiyo na maeneo jirani, hususan wale wanaojishughulisha na uvuvi.
0 Maoni