Karibu wafungwa 1,000 wakiume na wanawake wamejiunga na
vikosi vya mstari wa mbele vinavyokabiliana na moto wa nyika uliovunja rekodi
kusini mwa California.
Idadi ya wafungwa wanaoishiriki zoezi hilo la kuzima moto
sasa ni 939, chini ya mpango wa kujitolea unaoongozwa na Idara ya Urekebishaji
tabia ya California (CDCR).
Idadi ya wafungwa wanaoshiriki kuzima moto imeongezeka
kwa kazi tangu Jumanne, siku ambayo moto huo mkubwa ulisambaa baada ya
kushindikana kuudhibiti Los Angeles.
Zaidi ya majengo 10,000 yameharibiwa ekari 37 kuteketea
kwa moto, huku maelfu ya watumishi wa dharura wakifika Los Angeles kupambana na
moto.
0 Maoni