Idara ya Uhamiaji imetoa ufafanuzi kuhusu kupatiwa uraia
wa Tanzania wachezaji wa klabu ya Singida Black Stars, Emmanuel Kwame Keyekeh
(Ghana), Josephat Arthur Basa (Cote d'voire) na Muhamed Damara Camara wa
Guinea.
Taarifa ya idara hiyo imesema kuwa wachezaji hao watatu waliomba
uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura
ya 357, hivyo ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi.
0 Maoni