Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto
Mashaka Biteko amekutana na Waziri wa Nishati wa Umoja wa Visiwa vya Comoros,
Dkt Aboubacar Anli na kukubaliana maeneo kadhaa ya ushirikiano katika Sekta ya
Nishati.
Awali, Waziri wa Nishati wa Comoros alieleza umuhimu wa
ushirikiano kwenye sekta hiyo baina ya Comoro na Tanzania hususan kuanza
mazungumzo kwa ngazi ya wataalam ili kufanya upembuzi wa maeneo muhimu ya kuanzia hususan katika
uzalishaji na usambazaji umeme kwenye visiwa hivyo akieleza pia azma ya
Serikali yao kuzalisha umeme kwa vyanzo vya nishati ya mvuke (Geo Thermal)
inayopatikana kwa wingi visiswani humo.
Aidha, aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa maandalizi
mazuri na mkutano wa mafanikio wa Wakuu wa Nchi kuhusu Nishaki uliomalizika
hivi karibuni.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu Dkt.Biteko alieleza
utayari wa Tanzania katika kushirikiana na Comoro kwenye maeneo tajwa na
kuelekeza taratibu rasmi ili kuweza kufikiwa makubaliano rasmi kwenye Sekta ya
Nishati na uwezo na uzoefu wa Tanzania katika eneo hilo.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati, Dkt. Khatib Kazungu, Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi
Yakubu, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta za Nishati na
Maji, Bwana Andililo Tagalole, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) Mhandisi Boniface Nyamohanga Gisima, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania Bi Rosemary Jairo na Balozi wa
Comoro Nchini Tanzania Dkt Ahamada El Badaoui.
0 Maoni