Rais wa Marekani Donald Trump ameonya kuwa ataiwekea Urusi ushuru wa juu na vikwazo zaidi iwapo Rais Vladimir Putin atashindwa kumaliza vita nchini Ukraine.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump ameandika kuwa kushinikiza kutafuta suluhu la vita hivyo ni "kuipendelea sana" Urusi na rais wake.
Trump awali amesema kuwa atajadili kwa siku moja suluhisho la uvamizi kamili wa Urusi uliofanywa tangu Februari 2022.
Urusi bado haijajibu matamshi hayo, lakini maafisa
waandamizi wamesema katika siku za hivi karibuni kwamba kuna nafasi ndogo kwa
Moscow kujadiliana na utawala mpya wa Marekani.

0 Maoni