WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewasili Maputo nchini Msumbuji ambapo atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho wa Rais mteule wa Nchi hiyo Daniel Chapo utakaofanyika leo Januari 15, 2025.
Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa
asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO dhidi ya mpinzani wake Venancio
Mondlane aliyepata asilimia 20.32 katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 9,
2024.
Chapo anakuwa Rais wa tano wa Msumbiji, akichukua nafasi
ya Filipe Nyusi baada ya kukamilisha mihula miwili ya utawala wake.
Sherehe za uapisho zitafanyika katika uwanja wa
Independence (Uhuru) jijini Maputo.
0 Maoni