Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umemchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais mwaka 2025 kwa asilimia 100.
Akitangaza matokeo hayo jana msimamizi wa uchaguzi huo,
Dk Tulia Ackson amesema wajumbe 1,924 wote wamepiga kura ya ndiyo kwa Rais Dkt. Samia.
Kwa upande wa Zanzibar, Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi naye amepitishwa kuwa mgombea wa urais wa CCM katika uchaguzi wa 2025.
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Mkutano Mkuu una mamlaka ya
kumteua mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
0 Maoni