Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni
mgombea urais, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt.
Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025.
Rais Samia amempendekeza Dkt. Nchimbi jana Januari 19,
2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.
Awali Rais Dkt. Samia alimesema Makamu wa Rais Dkt.
Philip Mpango amemwandikia barua ya kuomba apumzike Umakamu wa Rais ambapo
amesema baada ya kutafakari ameridhia ombi hilo lakini kwa sasa Dkt. Mpango
ataendelea kuwa Makamu wa Rais hadi utakapofanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu
2025.
“Dkt. Philip
Mpango ndiye Makamu wa Rais miezi ya karibuni hapa amekuja kuniona kuniomba
apumzike, ana sababu kadhaa lakini sio za kazi, anasema yeye sasa ana miaka 68
na angependa kuishi zaidi kwahiyo naomba nipumzisheni, nikambishia bishia wiki
iliyopita hapa akanikabidhi barua yangu hii ya kujiuzulu na barua sikumjibu,
nilipoenda kwenye Kamati Kuu nikawaeleza hiyo hali na kwa pamoja wote
tukakubali tumpumzishe,” alisema Rais Dk. Samia.
0 Maoni