Waasi nchini Syria wametangaza kuwa Mji Mkuu wa Damascus upo huru kutoka mikononi mwa utawala wa muda mrefu wa rais Bashar al-Assad baada ya vikosi vya serikali kutimuliwa.
Waasi hao
wamesema kuwa taasisi za umma zitabakia chini ya usimamizi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mohammed Ghazi al-Jalali hadi hapo watakapokabidhiwa rasmi.
Taarifa
zinasema kuwa rais Bashar al-Assad, ameondoka Damascus kwa ndege kuelekea mahali
ambako hapajulikani.
Picha za
mjongeo ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha maelfu ya wafungwa wakiachiwa huru
kutoka gereza la wafungwa wakorofi la Saydnaya, ambapo wapinzani wa Assad
waliteswa na kuuawa.
Waziri Mkuu Ghazi
al-Jalali amesema kwamba wataitisha uchaguzi huru na haki, na kuongeza kuwa
ameongea na Kamanda wa waasi Abu Mohammed al-Jawlani kuhusu kipindi cha mpito.
0 Maoni