Kuelekea maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika, leo Desemba 7, 2024 Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imefanya usafi wa mazingira katika kituo cha Afya Kingolwira kilichopo Mkoani Morogoro.
Akizungumza
baada ya kumalizika kwa usafi wa kituo hicho cha afya, Afisa Mhifadhi Mkuu
ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhifadhi, Utafiti na Ujirani Mwema,
Omary Msangi amesema kuwa TAWA imetekeleza maelekezo yaliyotolewa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Waziri Mkuu, Mhe. Kasim Majaliwa alipozitaka
Taasisi zote za Serikali kushehereka maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru kwa
kufanya shughuli za kijamii.
"Sisi
kama TAWA katika kuunga mkono maelekezo ya Serikali tumechagua kuja katika
kituo cha Afya Kingolwira kwa lengo la kufanya usafi wa mazingira
yanayoizunguka kituo hiki." amesema Mhifadhi Msangi.
Aidha, Msangi ametoa rai kwa wananchi kuendelea
kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhifadhi rasilimali za wanyamapori,
misitu na mazingira kwa ujumla.
Naye,
Mwakilishi wa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kingolwira, Dkt. Leonard
Wambura ameishukuru TAWA kwa kununua vifaa vya usafi sambamba na kufanya usafi
wa mazingira katika kituo chao.
"Ninawashukuru
sana TAWA kwa nia yao nzuri ya kuja kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika
katika kituo chetu na tunawakaribisha tena wakati mwingine."
Aidha, Dkt.
alishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha vituo vya afya, vilevile alitoa rai kwa wananchi wa Morogoro kuja
kuendelea kuchangia damu kwa ajili ya kuendelea kuokoa Maisha ya mama na mtoto.
Ikumbukwe
hivi karibuni pamoja na maelekezo mengine Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa (Mb) alielekeza maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania yafanyike
Kwa ngazi ya Mikoa na Wilaya zote nchini Kwa kufanya shughuli za kijamii
zikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira katika maeneo ya kijamii kama vile
hospitali, masoko, kambi za wazee na wenye uhitaji maalumu.
0 Maoni