Waziri wa
Maji, Mhe. Jumaa H. Aweso (Mb) ametembelea na kufanya mazungumzo na Benki ya
EXIM ya Korea ambayo imefadhili utekelezaji wa miradi ya Majitaka nchini
Tanzania yenye jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 248.3 (Mkoa wa Dar es Salaam
90 $US milioni, Dodoma 70 $US million; na Iringa 88.3 $US million).
Katika
mazungumzo hayo, Makamu wa Rais wa Benki hiyo amesema kupitia EDCF na Mifuko
mingine Serikali ya Korea itaendelea kuisapoti Serikali ya Tanzania kupitia
Sekta ya Maji katika uwekezaji zaidi wa utekelezaji wa Miradi ya Maji.
Utelezaji wa
miradi hiyo utaimarisha huduma za Usafi wa Mazingira, kuondoa na kutibu
majitaka. Vilevile, Tanzania imepata msaada wa Dola za Kimarekani milioni 8
ambazo zitajenga mfumo wa kusimamia huduma za maji yaani Smart Water Management
System (SWMS) katika Mamlaka ya Maji Iringa kutoka Korea Environmental Industry
and Technology Institute (KEITI).
Pia, Kupitia
mfumo huo, IRUWASA itakuwa Mamlaka ya Maji ya kwanza Nchi kutumia mfumo huo
ambao utaongeza ufanisi katika kudhibiti upotevu wa maji, kuimarisha ukusanyaji
wa mapato na kuimarisha huduma ya maji.
Kupitia
ziara hiyo, Waziri Aweso ameimarisha ushirikiano na wadau wa maji Nchini Korea
ambao ni K-Water na makampuni mbalimbali hali ambayo imefungua fursa zaidi za
kushirikiana katika kujengea uwezo watumishi na Taasisi za Maji ikiwa ni pamoja
na kuandaa miradi na kutafuta fedha za utekelezaji.
0 Maoni