Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ona Machangu amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika utekelezaji wa afua mbalimbali za afya.
Dkt.
Machangu amebainisha hayo Jijini Dodoma wakati wa kuhitimisha Kikao cha Wadau
wanaotekeleza miradi mbalimbali ya afya ikiwemo afua za Elimu ya Afya.
"Tumekuwa
na Kikao kizuri sana na tunakuja na Mkakati wa pamoja katika kuhakikisha afua
za elimu ya Afya zinatekelezwa kwa ufanisi na upatikanaji wa taarifa na elimu
sahihi ya afya, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana wadau katika utekelezaji
wa afua hizo," amesema.
Beatrice
Joseph ni Mratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za afya,
kutoka Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau
kuanzia kwenye kupanga hadi utekelezaji.
"Serikali
hushirikiana na wadau kuanzia kupanga hadi utekelezaji na lengo ni kuhakikisha
afua za afya zinatekelezwa ipasavyo," amesema Beatrice.
Kwa upande
wake Mwakilishi wa Mradi wa USAID Afya yangu nyanda za juu Kusini Godfrey
Mwanakulya amesema Kikao hicho kina
mchango mkubwa katika utekelezaji wa afua za Elimu ya Afya hasa kwenye masuala
ya VVU na UKIMWI.
"Kikao
hiki kina umuhimu mkubwa katika utekelezaji wa afua za Afya kama sisi kwenye
Mradi wetu unaotekeleza afua za VVU na UKIMWI," amesema.
0 Maoni