Waasi wa Syria wadai kumtimua Rais Assad Damascus

 

Waasi nchini Syria wametangaza kuwa Mji Mkuu wa Damascus upo huru kutoka mikononi mwa utawala wa muda mrefu wa rais Bashar al-Assad baada ya vikosi vya serikali kutimuliwa.

Waasi hao wamesema kuwa taasisi za umma zitabakia chini ya usimamizi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mohammed Ghazi al-Jalali hadi hapo watakapokabidhiwa rasmi.

Taarifa zinasema kuwa rais Bashar al-Assad, ameondoka Damascus kwa ndege kuelekea mahali ambako hapajulikani.

Picha za mjongeo ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha maelfu ya wafungwa wakiachiwa huru kutoka gereza la wafungwa wakorofi la Saydnaya, ambapo wapinzani wa Assad waliteswa na kuuawa.

Waziri Mkuu Ghazi al-Jalali amesema kwamba wataitisha uchaguzi huru na haki, na kuongeza kuwa ameongea na Kamanda wa waasi Abu Mohammed al-Jawlani kuhusu kipindi cha mpito.

Chapisha Maoni

0 Maoni