Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
Taifa Freeman Mbowe amejikuta akiwa katika wakati mkumu wa kuamua kufuata
shinikizo la familia yake ama familia ya CHADEMA kufuatia kuibuka kwa wafuasi
wake wakimtaka agombee tena nafasi ya uenyekiti.
Wafuasi wa CHADEMA leo wamekusanyika nyumbani kwa mwenyeki
wa chama hicho, Freeman Mbowe, Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kumshawishi achukue fomu kuwania tena nafasi hiyo.
“Nimekuwa na wakati mgumu na familia yangu. Hakuna
kipindi familia yangu imenikalia mguu pande kama kipindi hiki, wananiambia baba
inatosha, toka achana na siasa rudi nyumbani uendelee na maisha mengine. Sasa
familia yangu nayo ina nguvu katika maisha yangu, lakini vilevile na familia ya
Chadema nayo ina nguvu sasa," amesema Mbowe na kuongeza,
“Ninaomba mniachie nimesikia rai yenu nimesikia hisia
zenu naheshimu hisia zenu naheshimu hisia za wengine wote ambao wamenifikia
nimefikiwa na watu wengi, nawaomba mnipe saa arobaini na nane (kuanzia leo
Jumatano) leo ni siku ya Jumatano nipeni Alhamisi, nipeni Ijumaa, Jumamosi
nitazungumza neno langu la mwisho na waandishi wa habari."
Amewaeleza wafuasi wake hao kwamba saa tano asubuhi siku
ya Jumamosi atazungumza na wahariri na waandishi waandamizi hapo hapo kutoa
kauli ya mwisho kuhusu mwenyekiti Mbowe naamua nini.
0 Maoni