Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa ametembelea banda la
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) lililopo katika Viwanja vya
Ukumbi wa AICC na kupata maelezo ya shunghuli nzima ya utalii mara baada ya
ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Tisa wa Mtandao unaohusisha Usimamizi wa
Rasilimali Watu katika Sekta za Umma Barani Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa
AICC jijini, Arusha.
Mkutano huo
umewakutanisha wataalamu kutoka nchi mbalimbali za Afrika kwa lengo la
kubadilishana uzoefu na mbinu za kuboresha usimamizi wa rasilimali watu katika
sekta za Umma za nchi hizo ili kuimalisha ufanisi na uwajibikaji kazini.
Mkutano ambao ulioanza tarehe 4, Novemba na unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 7,
Novemba 2024.
Akiwa katika
banda hilo la TANAPA jana Mhe. Majaliwa alirizishwa na maelezo ya kina
yaliyotolewa na Afisa Uhifadhi Daraja la I - Iddi Kaluse na CR II Caroline Msuya ya namna shirika hilo lilivyojizatiti
kuimalisha ulinzi wa maliasili na kutangaza utalii katika mikutano mbalimbali
hasa hii inayowakutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali.

0 Maoni