Wakazi wa kijiji cha Pongwe Msungura kilichoko Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani wamelishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa msaada mkubwa iliyoutoa kwa watoto wao.
Akizungumza
kwa niaba ya wazazi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Pongwe Msungura Bw Joel
Kajonga amesema JWTZ limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi na wanafunzi wa kijijini
hapo.
Naye Kamanda
wa Kikosi cha 8 kinachokwenda kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
Luteni Kanali Theofili Nguruwe amesema JWTZ ni jeshi la wananchi hivyo
litaendelea kutoa msaada kila itakapowezekana.
Msaada
uliotolewa shuleni hapo ni mahindi kwa ajili ya chakula, maharagwe, sukari,
madaftari, kalamu, viatu, mabegi vyote vikilenga kuongeza morari wa kusoma kwa
wanafunzi.
Mbali na
msaada huo pia wataalam wa afya wa JWZT waliweza kutoa matibabu na elimu ya
afya kwa wazazi wa kijiji hicho.



0 Maoni