Waziri Mkuu Majaliwa atembelea banda la TANAPA

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa ametembelea banda la Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) lililopo katika Viwanja vya Ukumbi wa AICC na kupata maelezo ya shunghuli nzima ya utalii mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Tisa wa Mtandao unaohusisha Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Sekta za Umma Barani Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa AICC jijini, Arusha.

Mkutano huo umewakutanisha wataalamu kutoka nchi mbalimbali za Afrika kwa lengo la kubadilishana uzoefu na mbinu za kuboresha usimamizi wa rasilimali watu katika sekta za Umma za nchi hizo ili kuimalisha ufanisi na uwajibikaji kazini. Mkutano ambao ulioanza tarehe 4, Novemba na unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 7, Novemba 2024.

Akiwa katika banda hilo la TANAPA jana Mhe. Majaliwa alirizishwa na maelezo ya kina yaliyotolewa na Afisa Uhifadhi Daraja la I - Iddi Kaluse na  CR II Caroline Msuya ya namna shirika hilo lilivyojizatiti kuimalisha ulinzi wa maliasili na kutangaza utalii katika mikutano mbalimbali hasa hii inayowakutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali.

Chapisha Maoni

0 Maoni