Timu ya
wavuta kamba (Me) ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) leo
Novemba 23, 2024 imeibuka mshindi wa 3 katika mchezo wa Kuvuta Kamba baada ya
kuishinda timu shindani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) katika
mashindano ya Mashirika ya Umma, Makampuni na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) ambayo
yanatarajiwa kufikia ukingoni Novemba 24, 2024 Jijini Tanga.
Akizungumza
mara baada ya ushindi huo, Kapteni wa timu ya Kamba (Me) ya TAWA Jumanne
Athumani amesema ushindi walioupata umekuwa ni faraja kubwa si tu Kwa wachezaji
hao bali Taasisi kwa ujumla kwani ni takribani miaka 10 sasa wamekuwa wakipambana
kufikia hatua hiyo bila mafanikio.
"Nimepende
kumshukuru Mungu kwa ushindi huu tulioupata, tumecheza na jirani zetu kabisa JU
01 Ngorongoro, mchezo ulikuwa mgumu na wa nguvu nyingi sana, mchezo ambao ni wa
jasho na damu," amesema Kapteni Jumanne Athumani.
"Kwa
mara ya Kwanza timu yetu imepambana kuweza kuleta kikombe hiki ambacho
tumekitafuta takribani miaka 10 bila kukipata, " ameongeza Jumanne.
Aidha
Jumanne ameishuru Menejimenti ya TAWA inayoongozwa na Kamishna wa Uhifadhi
Mabula Misungwi Nyanda Kwa kuwaamini na kuwapa fursa ya kushiriki mashindano
hayo ambayo wameyatumia vyema kutangaza utalii wa ndani Kwa vivutio
vinavyopatikana katika maeneo yaliyo chini ya usimamizi wa taasisi hiyo.
Mashindano
haya yaliyoshirikisha Mashirika mbalimbali ya Umma , Makampuni na Taasisi
Binafsi yalianza Novemba 10, 2024 na
yanatarajia kufikia ukingoni kesho Novemba 24, 2024 ambapo TAWA
ilishiriki katika michezo ya mpira wa miguu, Pete, Riadha na Mchezo
wa Kuvuta Kamba.
0 Maoni