Timu ya wanaume ya wavuta kamba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) leo Novemba 13, 2024 imeshinda mechi ya mchezo wa kuvuta kamba dhidi ya PSSSF Kwa mivuto miwili bila majibu (2 - 0) katika Mashindano ya Mashirika ya Umma, Makampuni na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea Mkoani Tanga.
Akizungumza
Kwa niaba ya wachezaji wa timu ya mchezo wa Kamba ya TAWA Nahodha wa timu hiyo
Jumanne Athumani ameishukuru Menejimenti ya taasisi hiyo Kwa kuwawezesha
kushiriki mashindano hayo ambayo pamoja na mambo mengine amesema wanayatumia
kuhamasisha utalii wa ndani Kwa vivutuo vya utalii vilivyopo TAWA.
Jumanne pia
ameushukuru uongozi na walimu wa timu ya kamba Kwa kuendelea kuwapa mbinu
mbalimbali za kuwakabili timu shindani katika mashindano hayo.
Kwa upande
wake Afisa Uhifadhi wa TAWA Taifa Liwewa amesema ushindi walioupata dhidi ya
PSSSF umekuwa chachu ya kuzidi kusonga mbele na kusisitiza kuwa malengo ya TAWA
katika mashindano hayo ni kufika fainali na kuchukua ubingwa.
TAWA
inashiriki mashindano hayo yaliyoanza Novemba 10, 2024 Jijini Tanga katika
michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa Pete na mchezo wa kuvuta
kamba ambapo inatajwa kufanya vyema katika michezo hiyo na kuonekana tishio
kila iingiapo dimbani.
Ushiriki wa
TAWA kwenye mashindano hayo sio tu unaleta ushindani Kwa timu pinzani, bali pia
unajenga mshikamano wa ndani na kuimarisha afya za wahifadhi.


 
 
 
 
 
 
 
 
0 Maoni