Serikali imepongeza
Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom kwa utoaji huduma za afya ikiwa ni
jitihada za kuunga Mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwapatia
huduma bora za afya wananchi.
Hayo
yamesemwa mbele ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Dayosisi ya Mbulu jana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi Mhe.
Geophrey Mizengo Pinda (Mb.) akimwakilisha Waziri wa Fedha. Mhe. Dkt Mwigulu
Nchemba kwenye Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Taasisi hiyo iliyopo
Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.
"Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imatambua mchango wa kanisa katika kuunga
mkono juhudi za serikali za kuwapatia wananchi huduma bora," amesema Mhe.
Pinda.
Mhe. Pinda
amewaasa wanafunzi wa Taasisi hiyo kutumia vema elimu wanayoipokea kwa kuendelea kujifunza kwa moyo wa kujitoa ili
kuongeza ubunifu na kuondoa changamoto zinazoikabili sekta ya Afya hapa nchini.
"Nawaasa
wanafunzi na wahitimu wa Taasisi hii Kuendelea kuwa na ari ya kujifunza,
ubunifu na kujitolea katika Kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya,"
amesema Mhe. Pinda.
Naye
Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Mbulu John Nade ameishukuru Serikali ya
awamu wa sita kwa kuiongezea taasisi hiyo nafasi za udahili wa wanafunzi kwa
mwaka wa Masomo 2024/25 na 2025/26.
"Tunaishukuru
sana Serikali ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kupitia ofisi ya rais Tamisemi
kwa uamuzi wake wa kuipa taasisi hii wanafunzi 60 kwa mwako 24/25 na Wanafunzi
40 kwa mwaka 2025/26 kwa fani ya Radiolojia," ameseme John Nade Msaidizi
wa Askofu.
Kwa Upande
Wake Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Fratei Gregory Massay amepongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha
kupeleka watumishi wa kutoa huduma katika Taaasisi Hiyo.
"Niishukuru
Serikali hasa Rais wetu wa Tanzania Mama yetu Dkt. Samia Suluhu hassan
ameshatusaidia watumishi watano mpaka sasa na sio hapa tu hata hosptali yetu
pia ametuletea," amesema Mhe. Fratei Mbunge wa Jimbo mbulu Vijijini.
Taasisi ya
Mafunzo ya Sayansi za afya Haydom ilianzishwa kwa lengo la kusaidia kujenga
uwezo wa kitaaluma na kutoa mafunzo bora katika nyanja mbalimbali za Sayansi za
afya na kuchangia kuboresha huduma za afya ndani na nje ya nchi.
0 Maoni