Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika
uwanja wa ndege wa Galeão Air Force Base Jijini Rio de Janeiro nchini Brazil
tarehe 16 Novemba, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20.
Rais Dkt.
Samia amealikwa na Rais wa Brazil Mhe. Luiz Inácio Lula da Silva ambapo pamoja
na mambo mengine, atashiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa
kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umaskini, kuchochea maendeleo
endelevu na matumizi ya nishati mbadala.
0 Maoni