Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan awalipia
viingilio watanzania wote kwenda uwanjani na kushuhudia mchezo wa Tanzania
dhidi ya Guinea, Mechi hiyo ya kufuzu kwa Mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON)
itachezwa leo jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam.
Akiwasilisha
taarifa hiyo, Dkt. Doto Biteko amesema Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
ameelekeza kuwa watu wote waingie uwanjani bure na hivyo wananchi wajitokeze
kwa wingi kwenda kuitia moyo timu yetu ya Taifa Stars na kwakweli imefanya
vizuri sana kwenye mechi iliyopita na tunaamini mechi hii tutashinda ili tuweze
kusonga mbele.

0 Maoni