Umoja wa
Mataifa (UN) umeonya kuwa mwaka 2024 utakuwa mwaka wenye joto kali katika
rekodi duniani, wakati mkutano wake wa mwaka wa hali ya hewa ukianza huko Baku.
Wakuu wa nchi
kutoka mataifa 200 wanatarajiwa kushiriki katika wiki mbili zijazo mkutano huo wa
COP29 unaofanyika kwenye taifa linalozalishaji mafuta la Azerbaijan.
Msisitizo utawekwa
katika kuona ni kwa namba gani nchi zinapanga kutekeleza mpango wa muda mrefu
wa kupunguza ongezeko la joto kwa nyuzi joto 1.5, kwa mujibu wa makubaliano ya Paris 2015.

0 Maoni