Mameneja wa
Mikoa wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) nchini wametakiwa
kutenga bajeti za matengenezo ya taa za barabarani ili kuhakikisha
zinatengenezwa pindi taa hizo zinapoharibika.
Agizo hilo
limetolewa na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati wa kikao kazi
na Watumishi wa TARURA Mkoa wa Mtwara kilichofanyika leo tarehe 11.11.2024
katika Ofisi ya Meneja wa TARURA Mkoa wa
Mtwara.
Mhandisi
Seff amesema kwamba Mameneja wa TARURA
wa Mikoa yote Nchini wanapaswa kutenga fedha za ukarabati wa taa kwenye bajeti
zao za kila mwaka ili wananchi waweze kutumia barabara hizo wakati wote hususan
usiku kwa shughuli za kiuchumi na kuongeza usalama wa watembea kwa miguu.
Mhandisi
Seff yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Mtwara ambapo baaada ya kuongea na
Watumishi wa TARURA-Mkoa alitembelea barabara za lami za ukanda wa viwanda za
EPZA zilizojengwa na TARURA mwaka 2021 zenye urefu wa kilometa 1.3 zilizopo
Mtwara Mjini.
Katika
barabara za ukanda wa EPZA Mtendaji Mkuu amemtaka Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Mtwara kuzifanyia matengenezo ya mara kwa mara
barabara hizo ikiwemo kufyeka nyasi ili kuzilinda zisiharibike na ziweze kudumu
kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa.
Barabara za
Ukanda wa Viwanda EPZA zimekuwa na tija kubwa kiuchumi kwa kuongeza kasi ya
ukuaji wa shughuli za viwanda katika Mkoa wa Mtwara na kuongeza ajira ikiwa ni
Utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala cha Mapundizi CCM ya mwaka 2020/2025.
Naye, Meneja
wa TARURA Mkoa wa Mtwara Mhandisi Zuena Mvungi amesema kuwa wamepokea maelelezo
yote na ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote ikiwemo ya kutenga fedha za
kukarabati taa za barabarani kwenye bajeti zao ili kuhakikisha wananchi
wanaendelea kuzitumia barabara hizo wakati wote na kwa usalama.


0 Maoni