Watu
wanapaswa kutumia muda wa dakika tano hadi 10 tu wakiwa chooni, kwa mujibu wa
Dk. Farah Manzour ambaye ni Profesa Msaidizi wa Tiba na Magonjwa ya Utumbo wa Tasisi
ya Tiba ya Stony Brook ya New York.
Dk. Manzour
amesema vyoo vya kukaa hukandamiza makalio, na kufanya eneo la kutolea haja (rectum)
kuwa katika eneo la chini, hivyo basi ukikaa muda mrefu mvuto wa kwenda
aridhini huongeza shinikizo kwa mzunguko wa damu.
Kutokana na
kukua kwa teknolojia watu huwa wanaenda vyooni na simu zao na kujikuta wakiwa
wanaangalia video, kusoma taarifa na vitabu ama kucheza gamu huku wakiwa
wanajisaidia na kujikuta wanajisahau na kukaa muda mrefu chooni.

0 Maoni