MADAKTARI WAONYA KUKAA MUDA MREFU CHOONI NI HATARI

 

Watu wanapaswa kutumia muda wa dakika tano hadi 10 tu wakiwa chooni, kwa mujibu wa Dk. Farah Manzour ambaye ni Profesa Msaidizi wa Tiba na Magonjwa ya Utumbo wa Tasisi ya Tiba ya Stony Brook ya New York.

Dk. Manzour amesema vyoo vya kukaa hukandamiza makalio, na kufanya eneo la kutolea haja (rectum) kuwa katika eneo la chini, hivyo basi ukikaa muda mrefu mvuto wa kwenda aridhini huongeza shinikizo kwa mzunguko wa damu.

Kutokana na kukua kwa teknolojia watu huwa wanaenda vyooni na simu zao na kujikuta wakiwa wanaangalia video, kusoma taarifa na vitabu ama kucheza gamu huku wakiwa wanajisaidia na kujikuta wanajisahau na kukaa muda mrefu chooni.

Chapisha Maoni

0 Maoni