Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Watu wa Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali ameziomba Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwenda kutoa huduma za kibingwa za matibabu kwa wananchi wa nchi hiyo.
Mhe. Ali alitoa ombi
lake hilo jana jijini Dar es Salaam wakati akiongea na viongozi wa Wizara ya
Afya pamoja na wa hospitali hizo katika
mkutano baina yao uliofanyika kwenye
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Waziri huyo wa Ulinzi alisema wataalamu wa hospitali hizo
wakienda nchini Comoro licha ya kuwasaidia wananchi kupata huduma pamoja na
kubadilisha ujuzi wa kazi na talaamu wenzao lakini pia wananchi wa Comoro
watafahamu wakija kutibiwa Tanzania gharama za matibabu zitakuwa kiasi gani na
watatibiwa na madaktari gani.
“Tanzania inapata dola za kimarekani milioni 100 kutoka
Comoro, hii inaonesha ushirikiano wetu ni wa umuhimu nichukue fursa hii
kuwaomba mfike Comoro ili muone namna
ambavyo mtaweza kutusaidia kuwatibu wananchi wetu, pia kuwajengea uwezo
wataalam wetu wa afya,” alisema Mhe. Ali.
Kwa upande wake Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Mhandisi Ismail Rumatila alisema Tanzania ilitia saini ya ushirikiano na
Jamhuri ya Watu wa Comoro Julai, 2024 katika sekta ya afya ulioruhusu
uhamishaji wa wagonjwa kutoka nchini humo kuletwa katika hospitali za afya za
umma za Tanzania kwa matibabu.
“Kupitia ushirikiano
huu taasisi zetu za JKCI, MOI na MNH watalazimika kwenda Comoro na kuona namna
bora ya kutoa matibabu kwa wananchi na kuwajengea uwezo watoa huduma wa Comoro
hatua hii ni utekelezaji wa agizo la Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la
kutaka Tanzania iwe kituo cha umahiri wa tiba utalii barani Afrika,”alisema Mhandisi Rumatila.
“Taasisi yetu kwa mwaka mmoja imeona wagonjwa 369 kutoka
nchi mbalimbali ikiwemo Comoro ni muhimu wacomoro wakatumia huduma zetu za
matibabu ya moyo kwani tuna wataalamu wa kutosha pamoja na vifaa tiba vya
kisasa pia mazingira yetu ni sawa na ya kwao,” alisema Dkt. Kisenge.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Asha Izina alimshukuru waziri huyo kwa kutembelea taasisi hiyo na kusema kuwa JKCI itawatuma wataalam.

0 Maoni