Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus
Balile amesema, taasisi hiyo inatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Nane (AGM)
kesho tarehe 7 Novemba 2024, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na vyombo vya habari leo katika Ofisi Kuu ya jukwaa hilo, Dar es Salaam amesema, mkutano huo utafunguliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa ambapo mada mbalimbali zitajadiliwa.
“Jukwaa letu ni la nchi nzima, leo wanachama wetu kutoka
maeneo mengine ya nchi wanafika na kesho ndio ufunguzi rasmi.”
“Pamoja na mambo mengine, tunatarajia kupokea wanachama wapya 25 ambao wametimiza vigezo vya uanachama,” amesema Balile.

0 Maoni