Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump ameshinda uchaguzi wa urais nchini Marekani.
Trump ameibuka mshindi baada ya kumshinda mpinzani wake
kutoka chama cha Democrats Bi. Kamala Harris.
Mgombea huyo wa Republican amepata ushindi mnono dhidi ya
Kamala Harris, unaomruhusu kurejea tena katika kiti cha urais wa Marekani.
Trump, ambaye alishinda uchaguzi wa 2016 na kupoteza wa 2020 dhidi ya Joe Biden, amemshinda Harris , ambaye alichukua nafasi ya Joe Biden kama mgombeaji wa Democrats.
Trump ameshinda katika majimbo muhimu ya North Carolina, Georgia, Pennsylvania na Wisconsin, ambayo yamempatia kiwango cha chini cha kura 270 za uchaguzi ambazo zilimemrejesha kuliongoza taifa hilo kubwa kiuchumi duniani.

0 Maoni